Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Majlisi ya Maombolezo kwa mnasaba wa kukumbuka na kuhuisha siku ya kuuwawa kishahidi Bibi Fatima Zahra (a.s), lilifanyika katika Msikiti wa Imam Zaynul Aabidin (a.s) uliopo Buyenzi, katika Jiji la Bujumbura, upande wa Magharibi mwa Burundi. Nchini Burundi. Tukio hilo lilihudhuriwa na waumini wengi wa kiume na wa kike ambao walikusanyika kuhuisha kumbukumbu hii chungu na kujifunza mafunzo muhimu kutokana na maisha ya Mwanamke huyu bora zaidi kuliko Wanawake wa ulimwengu mzima, bali mbora wa Wanawake wote wa Peponi. Majlisi ilianza kwa kisomo kitukufu cha Qur’ani Tukufu, kisha zikasomwa marsia na Maatam, na mashairi ya maombolezo yaliyoelezea kwa uchungu sehemu ya dhulma na mateso aliyoyapitia Sayyidat Fatima Zahra (a.s). Baadaye, khatibu alitoa hotuba yenye mwanga wa kiroho iliyoangazia fadhila za Bibi Zahra (a.s), nafasi yake ya kitablighi katika Uislamu, na msimamo wake wa kuutetea Uislamu na Uimamu. Baada ya hotuba, waumini walinyanyua mikono yao kwa dua na kuomba huruma za Mwenyezi Mungu, na Baraza (Majlis) likahitimishwa kwa kumswalia na kumuombea rehma na Amani Mtume wetu Muhammad na Aali zake Muhammad, sambamba na Dua ya kuomba kuruzukiwa Shafaa (Maombezi) ya Bibi Zahra (a.s) Siku ambayo mali wala watoto havitofaa chochote.

25 Novemba 2025 - 18:53

Your Comment

You are replying to: .
captcha